• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • APEC yampatia mtaalam wa China tuzo ya utafiti kuhusu mambo ya wanawake na uchumi

    (GMT+08:00) 2020-10-02 19:26:02

    Mtaalam wa China amepewa tuzo ya utafiti ya APEC ya mwaka 2020 ya wanawake wenye afya na uchumi mzuri, kwa mchango wake katika kuzuia saratani ya mlango wa uzazi.

    Mkurugenzi wa Idara ya saratani ya kituo cha taifa cha saratani na hospitali ya saratani ya academia ya sayansi za matibabu ya China Bibi Zhao Fanghui amepewa tuzo hiyo kutokana na utafiti wa kina kwenye matibabu ya kuzuia saratani ya mlango wa uzazi, kwenye nchi zenye uchumi wa chini na kati.

    Kwa mujibu wa Shirika la afya duniani WHO, saratani ya mlango wa uzazi ni ya nne miongoni mwa saratani zinazowaathiri wanawake wengi, hata hivyo inaweza kuzuiliwa kwa mbinu za upimaji na chanjo.

    Tuzo hiyo ilizinduliwa mwaka jana nchini Chile, na hutolewa kwa watu wanaowawezesha watunga sera na viongozi wa biashara kutambua na kutekeleza hatua zinazoboresha afya ya wanawake.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako