• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • ZANZIBAR: CORONA YAPUNGUZA WATALII

    (GMT+08:00) 2020-10-05 16:34:26

    Jumla ya wageni 4,366 wameingia nchini Zanzibar mwezi Agosti mwaka huu, ikilinganisha na idadi ya wageni 68,163 kwa mwezi Agosti mwaka uliopita ambapo idadi ya uingiaji wa wageni imepungua.

    Takwimu hizo zilitolewa na Mkuu wa Kitengo cha Takwimu za Utalii, Abdulmalik Bakar Ali wakati akitoa taarifa kwa vyombo vya habari katika ofisi ya Mtakwimu mkuu wa serikali, Mazizini.

    Aidha alisema asilimia 61.7 ya wageni walioingia nchini mwezi uliopita walitoka bara la Ulaya sawa na ongezeko la asilimia 35.2 ukilinganisha na mwezi wa Julai mwaka huu ambapo jumla ya wageni walioingia nchini walikuwa 3,079.

    Abdulmalik alizitaja nchi iliyoongoza kuleta wageni ni Ufaransa ambapo ilichangia asilimia 15.3 ya wageni waliongia nchini ikifuatiwa na Marekani iliyochangia kwa asilimia 9.2.

    Alibainisha kuwa kwa mwezi Agosti asilimia 77.0 ya wageni walipita uwanja wa ndege na asilimia 23.0 walipitia bandarini kati ya hao asilimia 45.4 walikuwa wanaume na wanawake walikuwa ni asilimia 44.6.

    Meneja Benki Kuu ya Tanzania (BoT) tawi la Zanzibar, Moto Nwinganele, alisema serikali imefanya uchunguzi kupitia wizara ya fedha na kubaini changamoto ya kiuchumi zilizotokana na maradhi ya corona. Alisema katika kutatua changamoto hiyo serikali ilipunguza baadhi ya kodi na nyengine kuzuiliwa kulipa kabisa mpaka hali ya kiuchumi itakapokaa sawa kwa kuwasaidia wawekezaji wanaotegemea sekta ya utalii.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako