• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • BUNGE LA AFRIKA MASHARIKI LAIDHINISHA BAJETI YA EAC.

    (GMT+08:00) 2020-10-05 16:36:02

    Bunge la Afrika Mashariki limeidhinisha makadirio ya bajeti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa mwaka wa fedha 2020/21, kiasi cha dola milioni 104 baada ya mjadala mkali wa siku nzima uliofanywa na mkutano wa kawaida.

    Bunge pia lilipitisha Muswada wa Matumizi ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, 2020, na marekebisho, ya bajeti ya ukanda huu, kwa dola zaidi ya milioni saba ikizingatiwa makadirio ya bajeti ya awali ya jumla ya dola milioni 97.6 kama ilivyowasilishwa wiki moja iliyopita na Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri,Manase Nshuti.

    Muswada wa awali wa Matumizi ya EAC, 2020 ulipendekeza jumla ya $ 97,669,708 (ikilinganishwa na $ 111,450,529 kwa mwaka wa fedha 2019/2020) kama ilivyopendekezwa na Nshuti wiki iliyopita.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako