• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • UN: AFRIKA YAPOTEZA MABILIONI YA DOLA KWA FEDHA HARAMU KILA MWAKA.

    (GMT+08:00) 2020-10-05 16:36:44

    Utafiti uliondeshwa na Umoja wa Mataifa, umeonyesha bara la Afrika linapoteza takriban dola billioni 89 kila mwaka katika mtiririko haramu wa fedha kama vile ukwepaji kodi na wizi. Ripoti hiyo yenye kurasa 248, iliyotolewa wiki jana, imetolewa na bodi ya Umoja wa Mataifa ya biashara na maendeleo UNCTAD.

    Ripoti inaeleza fedha zinazopotea ni zaidi ya zile ambazo bara la Afrika inazipata katika misaada ya maendeleo, na makadirio hayo ni makubwa zaidi kuliko ya awali. Takriban nusu ya hasara ya dola billioni 88.6 kwa mwaka ni mapato ya bidhaa zinazouzwa nje kama vile dhahabu, almasi na madini ya platinum, kwa mujibu wa ripoti ya UNCTAD.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako