• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Serikali ya Hong Kong yapinga taarifa iliyotolewa na Marekani

    (GMT+08:00) 2020-10-05 17:36:49

    Serikali ya Mkoa wa Utawala Maalum wa Hong Kong, China (HKSAR) imepinga vikali taarifa iliyotolewa na wizara ya mambo ya nje ya Marekani jumamosi iliyopita kuhusiana na hatua ya polisi wa Hong Kong ya kuwakamata washukiwa.

    Msemaji wa serikali ya Hong Kong amesema inasikitisha kuwa maafisa wa ngazi ya juu wa Marekani wanazidi kufanya makosa kwa kutekeleza vigezo viwili tofauti, akielezea matamshi yasiyo ya kweli kuhusu vitendo vya utekelezaji wa sheria huko Hong Kong.

    Serikali hiyo imeikumbusha Marekani kwamba Hong Kong ni sehemu ya Jamhuri ya Watu wa China, na mambo yanayohusu Hong Kong ni mambo ya ndani ya China, hivyo serikali za nchi nyingine zinapaswa kuacha kueneza taarifa zisizo sahihi na kutoingilia kati kwa njia yoyote mambo yanayohusu Hong Kong.

    Msemaji huyo pia ameongeza kwamba, kukamatwa kwa washukiwa kunafuata sheria na ni muhimu katika kudumisha amani na utulivu katika jamii, na kulinda maisha na mali za wakazi wa Hong Kong.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako