• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yaandikisha zaidi ya watalii milioni 4 wa ndani katika Siku ya Taifa

    (GMT+08:00) 2020-10-05 17:37:08

    Wizara ya Utalii na Utamaduni ya China imesema, watalii milioni 425 wa ndani wametembelea vivutio mbalimbali vya utalii nchini katika siku nne za mwanzo za mapumziko ya Siku ya Taifa, na kuingiza dola za kimarekani bilioni 45.8.

    China ilianza kusherehekea siku ya taifa Oktoba Mosi, ambapo mwaka huu mapumziko hayo imeongezwa hadi Octoba 8. Hii ni likizo ya kwanza ya kitaifa tangu China ifungue safari za kitalii kati ya mikoa mwezi wa Julai baada ya kukumbwa na janga la virusi vya Corona.

    Zaidi ya vivutio vya utalii 1,000 kote nchini China vimeondoa au kupunguza ada za malipo kwa watalii wakati wa likizo hiyo. Sekta ya utalii nchini China imeanza tena kuimarika kutokana na sera nzuri za kuboresha utalii pamoja na mafanikio katika kudhibiti virusi vya Corona.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako