• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • IMF yataka uwekezaji zaidi kwenye miundombinu ili kukuza uchumi baada ya janga la COVID-19

    (GMT+08:00) 2020-10-06 15:33:34

    Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) limesema nchi wanachama zinapaswa kuchukua fursa ya riba ndogo kuwekeza katika miundombinu ili kuchochea ukuaji baada ya janga la virusi vya Corona na kubadili mwelekeo kuwa wa nishati ya kijani.

    Shirika hilo limesema kuwa utafiti umeonyesha kuwa uwekezaji wa umma katika miundombinu ikiwemo mfumo wa afya, miundombinu ya kidijitali na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi unaweza kuleta faida zaidi.

    Jumatatu wiki hii, Shirika hilo lilipitisha msaawa mpya wa dharura kwa nchi 28 zilizo masikini zaidi duniani zikiwemo Rwanda, Tanzania na Burundi ili kuzisaidia kupunguza madeni yao na kukabiliana na athari za janga la virusi vya Corona.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako