• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yatoa wito wa kuondolewa kwa vikwazo vya upande mmoja

    (GMT+08:00) 2020-10-06 17:10:03

    Mwakilishi wa kudumu wa China kwenye Umoja wa Mataifa Balozi Zhang Jun ameikosoa Marekani na nchi za Magharibi kwa kukiuka haki za binadamu, na kutoa wito wa kuondolewa mara moja kwa vikwazo vya upande mmoja.

    Balozi Zhang Jun amesema hayo alipotoa taarifa ya pamoja kwa niaba ya nchi 26, zikiwamo Angola, Burundi, na Cameroon, katika mjadala wa Kamati ya tatu ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa. Amesisitiza kwamba janga la virusi vya Corona linaendelea kuathiri vibaya nchi zote, haswa nchi zinazoendelea, na kuongeza kuwa, ili kurudi katika hali ya kawaida baada ya janga hilo, umoja na ushirikiano wa kimataifa unahitajika. Lakini amesema vitendo vya upande mmoja kulazimisha pande nyingine vinashuhudiwa, ambavyo ni kinyume na azma na kanuni za Katiba ya Umoja wa Mataifa, sheria ya kimataifa, mfumo wa pande nyingi na kanuni za msingi za uhusiano wa kimataifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako