• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wakazi milioni 285 vijijini nchini China watumia mtandao

    (GMT+08:00) 2020-10-06 17:10:37

    Ripoti mpya iliyotolewa hivi karibuni imeonyesha kuwa, hadi kufikia mwezi Juni mwaka huu, watu milioni 285 wanaoishi katika maeneo ya vijijini nchini China wanatumia mtandao, idadi ambayo ni asilimia 30 ya watu wote wa China.

    Idadi ya watumiaji wa mtandao vijijini nchini China imeongezeka kwa zaidi ya milioni 30 kuanzia mwezi Machi, na kupunguza pengo la matumizi ya mtandao kwa wakazi vijijini na mijini.

    Ripoti hiyo imeongeza kuwa, mtandao umesaidia sana katika kazi ya kuondokana na umaskini nchini China. Pia ripoti hiyo inaonesha kwamba, matangazo ya biashara kupitia mtandao wa internet yaliongezeka sana katika nusu ya kwanza mwaka huu. Kufikia mwezi Juni, idadi ya watu wanaotangaza biashara zao mubashara kupitia mtandao nchini China ilifikia milioni 309, ikiwa ni ongezeko la asilimia 16.7 kuliko ile ya mwezi Machi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako