• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Marekani, Russia na Ufaransa zatoa wito wa kusitishwa mara moja kwa mapigano katika eneo la Nagorno-Karabakh

    (GMT+08:00) 2020-10-06 17:10:59

    Wanadiplomasia waandamizi wa Marekani, Russia na Ufaransa wametoa wito wa kusitishwa mara moja kwa mapigano yanayoendelea katika eneo la ya Nagorno-Karabakh, ambapo miji muhimu ilishambuliwa.

    Nchi hizo tatu ambazo zinaongoza timu ya upatanishi zimeshindwa kutoa suluhisho la kisiasa, na taarifa ya pamoja iliyotolewa na mawaziri wa mambo ya nje wa nchi hizo tatu imelaani vikali mapigano yanayoendelea ndani na nje ya eneo la Nagorno-Karabakh kugombania ardhi iliyo kati ya nchi za Armenia na Azerbaijan.

    Taarifa hiyo imeeleza kuwa mashambulizi yanayoendelea yanalenga makazi ya raia kwenye maeneo nje ya maeneo ya mapigano, na kuongeza kuwa, Marekani, Russia na Ufaransa zitaendelea kushirikiana na Armenia na Azerbaijan, kuzihimiza kushiriki kwenye mchakato wa kutafuta suluhisho la kudumu kwa kufuata kanuni za msingi na nyaraka husika za kimataifa zinazotambuliwa na pande zote mbili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako