• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Muujiza wa China wachangia kazi ya uondokanaji umaskni duniani

    (GMT+08:00) 2020-10-06 17:15:51

    Takwimu zilizotolewa na Benki ya Dunia (WB) zinaonyesha kuwa, mafanikio yaliyopatikana nchini China yamechangia asilimia 70 ya juhudi za dunia katika kuondokana na umaskini. Ni katika miaka minane tu kuanzia mwaka 2012 hadi 2019, idadi ya watu maskini nchini China imepungua kwa milioni 90.

    Hadi itakapofika mwisho wa mwaka huu, China inatarajia kutimiza lengo lililowekwa la kuondoa kabisa umaskini, hivyo kutimiza lengo lililowekwa na Umoja wa Mataifa katika Ajenda ya Maendeleo Endelevu ya mwaka 2030. Ikiwa ni nchi inayoendelea yenye watu bilioni 1.4, muujiza huo ni mchango mkubwa kwa kazi ya kuondokana na umaskini duniani.

    Hivi sasa janga la virusi vya Corona ni changamoto kubwa kwa juhudi za binadamu za kuondokana na umaskini. Kwa mujibu wa makadirio yaliyotolewa katika ripoti ya Umoja wa Mataifa, mwaka huu, watu milioni 71 duniani watarudi katika umaskini uliokithiri. Katika mkutano wa kilele wa maadhimisho ya miaka 75 ya kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa uliofanyika hivi karibuni, rais Xi Jinping wa China kwa mara nyingine tena alitoa wito wa kutoa kipaumbele katika suala la maendeleo, ambalo ni ufumbuzi unaoweza kusaidia binadamu kukabiliana na msukosuko wa hivi sasa.

    Katika kongamano lililofanyika hivi majuzi la kujadili malengo ya maendeleo endelevu na uzoefu wa China katika kuondokana na umaskini, wataalamu wa nchi mbalimbali walipendekeza kujifunza kwa China. Mwanadiplomasia mstaafu wa Afrika Kusini Bw Gert Grobler alisema, China imefanya kazi kubwa ya kusaidia maendeleo barani Afrika, na nchi za Afrika zinavutiwa na mafanikio ya China na kujifunza mengi kutoka China.

    Pamoja na juhudi za kuondokana na umaskini, China pia inajituma katika ushirikiano wa kimataifa, na kusaidia nchi nyingine kupitia kubadilishana wataalamu, kufanya utafiti kwa pamja na kutoa msaada wa kiteknolojia. Miradi mingi ya kuondokana na umaskni kati ya China na nchi nyingine zinazoendelea imetekelezwa katika mabara ya Afrika, Asia na Latin Amerika.

    Dunia bado haijadhibiti kuenea kwa virusi vya Corona, na juhudi za kutimiza malengo ya maendeleo endelevu ya Umoja wa Mataifa ya mwaka 2030 zinakabiliwa na changamoto mbalimbali. Kutokana na hali hii, binadamu hana chaguo lingine ila tu kufanya bidii zaidi na kuendelea kusonga mbele kuelekea lengo kuu la kuondoa kabisa umaskini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako