• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Kyrgyzstan atoa wito wa utulivu wa kijamii wakati maandamano yakiendelea nchini humo

    (GMT+08:00) 2020-10-06 18:24:32

    Rais wa Kyrgyzstan Sooronbai Jeenbekov amehutubia taifa hilo leo baada ya waandamanaji kupambana na vikosi vya usalama, akisema utulivu wa kijamii ni wa thamani zaidi.

    Katika hotuba hiyo, rais Jeenbekov amesema, kutumia matokeo ya uchaguzi kama chanzo cha vurugu ni ukiukaji wa utaratibu wa kijamii, na kuwataka wananchi waendelee kuwa na utulivu. Pia amewataka viongozi wa vyama vya siasa kuwatuliza wafuasi wao na kuwaondoa katika maeneo waliyokusanyika.

    Rais huyo amependekeza kuwa Tume ya Uchaguzi nchini humo (CEC) inapaswa kuchunguza kwa makini tuhuma za ukiukaji wa sheria za uchaguzi, na kama ni lazima, kufuta matokeo ya uchaguzi wa wabunge.

    Mapema leo, waandamanaji ambao hawakuridhika na matokeo ya awali ya uchaguzi huo walivamia na kukalia jengo la bunge na jengo la Kamati ya Usalama wa Taifa nchini humo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako