• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Biden asema mjadala mwingine usifanywe kama Trump bado atakuwa na COVID-19

    (GMT+08:00) 2020-10-07 18:18:38

    Mgombea wa urais kwa tiketi ya chama cha Democratic Joe Biden amesema mjadala unaofuata wa kuwania urais haupaswi kufanyika kama mgombea wa Republican ambaye ni rais wa Marekani Donald Trump, bado atakuwa na COVID-19.

    Wagombea hao walipokutana kwenye mjadala wao wa kwanza Sept. 29 huko Cleveland, Ohio, hawakushikana mikono na kulikuwa na umbali kati yao, lakini si Biden wala Trump aliyevaa barakoa kwenye jukwaa.

    Wakati huohuo wajumbe wa wanadhimu wakuu wa pamoja wa Marekani akiwemo Mwenyekiti Mark Milley, wameripotiwa kuwepo kwenye karantini baada ya kupata COVID-19, huku maambukizi ya ikulu ya White House Marekani yakiendelea kuongezeka.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako