• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Jaribio la Marekani na nchi nyingine la kuchafua hali ya haki za binadamu lashindwa tena kwenye Umoja wa Mataifa

    (GMT+08:00) 2020-10-07 18:19:46

    Jaribio la Marekani na nchi nyingine kadhaa la kuchafua hali ya haki za binadamu mkoani Xinjiang na Hong Kong limeshindwa tena baada ya nchi karibu 70 kujitokeza kuiunga mkono China katika mjadala mkuu wa Kamati ya Tatu ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.

    Balozi wa China kwenye Umoja wa Mataifa Bw. Zhang Jun amepinga shutuma zisizo na msingi zilizotolewa na Marekani, Ujerumani, Uingereza na nchi nyingine kadhaa na vitendo vya kuingilia kati mambo ya ndani ya China kwa kutumia jina la haki za binadamu na kuchochea mgogoro kati ya nchi wanachama.

    Karibu nchi 70 ziliitikia msimamo huo wa China, na kwamba Pakistan, Cuba na Kuwait kila moja ilitoa taarifa ya pamoja ikiziwakilisha nchi nyingine kuunga mkono juhudi za China katika kulinda usalama wa Hong Kong, na kupambana na ugaidi na msimamo mkali mkoani Xinjiang.

    Akizungumzia hilo, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Bibi Hua Chunying leo hapa Beijing amesema China inapinga kithabiti mtu yeyote na nchi yoyote kuleta ukosefu wa utulivu, mfarakano na ghasia nchini China, kupinga kutatiza kisiasa mambo ya Hong Kong na Xinjiang na kuingilia kati masuala ya China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako