• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Covid-19 kuingiza kwenye umaskini uliokithiri,yasema Benki ya Dunia

    (GMT+08:00) 2020-10-08 19:04:12

    Benki ya Dunia inasema umaskini uliokithiri duniani unatarajiwa kuongezeka mwaka huu wa 2020,kwa mara ya kwanza ndani ya kipindi cha zaidi ya miaka 20.

    Benki hiyo imesema kuwa janga la Covid-19 litaongeza nguvu za mizozo na mabadiliko ya hali ya hewa,ambayo tayari yalikuwa yanaonyesha maendeleo ya kupunguza umaskini.

    Janga la korona linakadiriwa kusukuma watu milioni 88 hadi milioni 115 kwenye umaskini uliokithiri mwaka huu,huku watu wote kwa ujumla wakikadiriwa kuwa milioni 150 kufikia mwaka 2021,kulingana na makali ya mpunguo wa uchumi.

    Umaskini uliokithiri,unaotajwa kuwa ni kuishi chini ya $1.90 kwa siku ,huenda ukaathiri kati ya asilimia 9.1 na asilimia 9.4 ya idadi ya watu duniani mwaka 2020.

    Ikiwa janga la korona halingefika ulimwenguni,kiwango cha umaskini kilitarajiwa kushuka hadi asilimia 7.9 mwaka 2020.

    Ripoti hiyo aidha inaonyesha watu wengi maskini watapatikana katika nchi ambazo tayari zina viwango vikubwa vya umaskini.

    Kenya ni miongoni mwa nchi ambazo raia wanaishi katika kiwango kikubwa cha umaskini.

    Kulingana na Benki ya Dunia,idadi ya nchi zenye uchumi wa kati zitakuwa na watu wengi ambao wataangukia kwenye umaskini uliokithiri.

    Ripoti hiyo inakadiria kuwa takriban asilimia 82 ya watakaoathirika na umaskini uliokithiri ni watu walioko kwenye nchi zenye kipato cha kati.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako