• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania na Malawi zakubaliana kushirikiana ili kuboresha biashara yao

    (GMT+08:00) 2020-10-08 19:05:02

    Tanzania na Malawi zimekubaliana kushirikiana kuboresha sekta za usafirishaji, uvuvi, madini, nishati, utalii na kilimo.

    Makubaliano hayo yalitangazwa jana Ikulu jijini Dar es Salaam wakati wa hafla maalum iliyohusisha marais wa nchi hizo mbili, mwenyeji Dk. John Magufuli na Rais Lazarus Chakwera aliyezuru nchini kwa ziara ya siku tatu.

    Rais Magufuli alimshukuru Rais Chakwera kwa kuitembelea Tanzania na kuwa nchi ya tatu kutembelewa barani Afrika kwa kiongozi mpya wa Malawi baada ya Burundi na Uganda tangu aingie madarakani.

    Katika hafla hiyo, Rais Magufuli alisema nchi hizo mbili zina historia ya undugu kutokana na mwingiliano wa watu wake katika shughuli mbalimbali ikiwamo biashara.

    Rais Magufuli alisema kuna kampuni nane kutoka Malawi zimewekeza nchini na kutoa ajira kwa Watanzania 390 na kwamba zipo kampuni zilizowekeza Malawi kutoka nchini.

    Alisema usafiri ukiimarika baina ya nchi hizo mbili, utafanya biashara ifanyike kwa urahisi na hivyo nchi hizo zijiikite kwenye uhusiano wa kibiashara na mizigo ya Malawi kupitia Tanzania itaongezeka.

    Rais Chakwera alisema bandari za nchi hizo mbili zikishirikiana, itasaidia kukuza uchumi wa nchi hizo.

    Rais Chakwera pia alieleza kuguswa kwa namna Tanzania ilivyodhibiti sekta ya madini na kuongeza mapato yake, akisisitiza ni mfano wa kuigwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako