• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yakanusha shutuma zisizo na msingi za Marekani katika Umoja wa Mataifa

    (GMT+08:00) 2020-10-08 19:11:06

    Naibu balozi wa China kwenye Umoja wa Mataifa Bw.Dai Bing amekanusha na kulalamikia shutuma zisizo na msingi zilizotolewa na Marekani dhidi ya China katika masuala ya ugonjwa wa Corona na haki za binadamu.

    Balozi Dai amesema shutuma hizo zinalenga kuchochea mapambano na kukidhi malengo ya kisiasa ya ndani ya Marekani, na kwamba kuipaka matope na kuitupia lawama China katika suala la ugonjwa wa Corona ni kitendo kisicho sahihi na pia ni cha bure. Amesema Marekani inatakiwa kuwaeleza wananchi wake jinsi hali ya maambukizi ya virusi vya Corona nchini humo inavyokuwa mbaya kiasi cha kuongoza duniani kwa idadi ya watu walioambukizwa na waliofariki dunia kwa ugonjwa huo.

    Katika suala la haki za binadamu, balozi Dai amesema watu wa China wana sauti zaidi kuhusu jinsi hali ya haki za binadamu ilivyo nchini mwao, na ni ndoto ya mchana kwa nchi yoyote kuzuia maendeleo ya China. Ameitaka Marekani iachane na fikra ya vita baridi na upendeleo wa kiitikadi, kutambua maendeleo makubwa ya China katika suala la haki za binadamu na kuacha kueneza uwongo na "virusi vya kisiasa".

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako