• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China kushuhudia ongezeko kubwa la safari za kurudi wakati sikukuu inapomalizika

    (GMT+08:00) 2020-10-08 19:11:43

    China itashuhudia ongezeko kubwa wasafiri wanaorudi baada ya kumaliza mapumziko ya siku nane ya siku ya taifa.

    Kwa mujibu wa shirika la reli la taifa la China, leo inatarajiwa kuwa safari za treni zinazokadiriwa kuwa milioni 13, na treni 1,234 za ziada zimetumiwa ili kushughulikia ongezeko kubwa la watalii na kutembelea familia.

    Shirika hilo limesema shughuli za usafiri zimeendelea kwa utulivu na taratibu katika kipindi cha sikukuu hiyo, na kwamba safari za treni za kila siku hapa China zilifikia milioni 10 kwa siku nane mfululizo.

    China inasherehekea siku ya Taifa tarehe mosi Oktoba, na mwaka huu mapumziko yamefika siku nane kwa kujumuisha na Sikukuu ya Jadi ya Mwezi inayoangukia tarehe 15 mwezi wa nane kwa kalenda ya kilimo ya China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako