• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kikao maalum cha UM chahimiza hatua za kuleta ushindi dhidi ya COVID-19

    (GMT+08:00) 2020-10-08 19:12:53

    Mwenyekiti wa baraza kuu la 75 la Umoja wa Mataifa Bw. Volkan Bozkir, amesema lengo la kikao maalum kijacho kuhusu kupambana na COVID-19 ni kuhimiza hatua za jumuiya ya kimataifa kushinda COVID-19 na kusaidia kupunguza athari zake za kijamii, kibinadamu na kiuchumi.

    Imefahamika kuwa kwenye kikao kilichopita cha baraza hilo kila mjumbe alizungumzia madhara ya ugonjwa huo, na kuna haja kwa nchi zote kushughulikia changamoto hii kwa pamoja.

    Akiongea kwenye mkutano kuhusu maandalizi ya kikao cha baraza hilo Bw. Bozkir pia amesisitiza

    kuwa mshikamano na ushirikiano ni muhimu katika kushinda changamoto hii ambayo haijawahi kutokea, na kuwa kikao hicho maalum kinatoa fursa ya kihistoria na lazima kikao kifanyike haraka iwezekanavyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako