• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Usafirishaji wa abiria na mizigo kwenye reli ya SGR ya Kenya waongezeka

  (GMT+08:00) 2020-10-08 19:16:48

  Idadi ya abiria na kiasi cha mizigo iliyosafirishwa kwenye treni ya SGR ya Kenya (SGR) vilidumisha ongezeko la kasi katika mwezi Agosti, ikionyesha kuongezeka kwa mahitaji ya huduma hiyo baada ya kufunguliwa kwa uchumi wa nchi hiyo kutokana na kupungua kwa maambukizi ya COVID-19.

  Takwimu kutoka Shirika la Reli la Kenya (KRC) zinaonyesha kuwa abiria 32,641 walitumia usafiri wa treni hiyo katika mwezi Agosti, wakiwa wameongezeka kutoka abiria 19,502 wa mwezi Julai.

  Kuongezeka mara dufu kwa idadi ya abiria wanaosafiri kati ya Nairobi na Mombasa kunaonyesha matarajio mazuri kwenye sekta ya utalii ya Kenya, ambayo kwa sasa inategemea zaidi watalii wa ndani.

  Mapato yaliyokusanywa kutokana na huduma ya usafiri wa abiria, pia yaliongezeka kufikia hadi shilingi milioni 39.5 (karibu dola za Kimarekani laki 3.65) kwa mwezi, kutoka dola laki 2.1 za mwezi Julai. Bidhaa za kusafirishwa nje ya nchi kupitia reli hiyo pia zikiongezeka kutoka tani laki 3.16 na kufikia tani laki 3.5. Katika mwezi huo wa Agosti shehena ya bidhaa za kuagizwa kutoka nje zilizosafirishwa kwa reli hiyo ilipungua kidogo na kuwa tani milioni 2.18, kutoka tani milioni 2.46.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako