• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wagombea wawili wanawake waingia kwenye raundi ya mwisho kugombea uongozi wa WTO

    (GMT+08:00) 2020-10-09 09:25:51

    Bodi ya Shirika la biashara duniani (WTO) imetangaza kuwa baada ya raundi mbili za mazungumzo, wanachama wa bodi hiyo wameamua mkurugenzi mpya wa shirika hilo atachuguliwa kati ya wagombea wawili wanawake. Hii inaonesha kuwa shirika la WTO litakuwa na mkurugenzi wa kwanza mwanamke tangu lianzishwe miaka 25 iliyopita.

    Bibi Ngozi Okonjo-Iweala kutoka Nigeria na Bibi Yoo Myung-hee kutoka Korea Kusini wameingia kwenye raundi ya mwisho, ambayo itafanyika tarehe 19 hadi 27 mwezi Oktoba.

    Bibi Ngozi Okonjo-Iweala aliwahi kuwa waziri wa fedha na waziri wa mambo ya nje wa Nigeria, pia aliwahi kufanya kazi katika Benki ya Dunia kwa miaka 25. Bibi Yoo Myung-hee ni waziri wa mawasiliano ya biashara wa Korea Kusini, ambaye aliiwakilisha nchi yake mara nyingi kwenye mazungumzo muhimu ya kimataifa .

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako