• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Trump akataa kushirki mdahalo wa pili wa urais utakaofanyika kwa njia ya video

    (GMT+08:00) 2020-10-09 09:26:25

    Tume ya mdahalo wa urais ya Marekani imesema mdahalo wa pili wa urais utafanyika kwa njia ya video, lakini Rais Donald Trump wa Marekani amesema hatashiriki kwenye mdahalo huo.

    Tume hiyo jana ilitoa taarifa ikisema mdahalo wa pili utafanyika tarehe 15, na ili kuhakikisha afya na usalama wa pande mbalimbali, rais Trump na mgombea kutoka Chama cha Democrats Bw Joe Biden watafanya mdahalo kwa njia ya video wakiwa mahali tofauti.

    Muda mfupi baada ya kutolewa kwa taarifa hiyo, rais Trump alisema kwenye mahojiano na televisheni ya FOX, kuwa hatakubali wala hatashiriki kwenye mdahalo utakaofanyika kwa njia ya video, ambao unalenga kumlinda Joe Biden. Rais Trump amesema hataambukiza watu wengine, pia anajisikia vizuri na anaweza kuendelea na kampeni.

    .

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako