• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ofisa ajulisha uzoefu wa China wa kupunguza umaskini kwenye Baraza la Haki za Binadamu UM

    (GMT+08:00) 2020-10-09 09:29:14

    Mkutano wa Baraza la kijamii la Baraza la Haki za Binadamu la Mwaka 2020 ulifunguliwa jana huko Geneva, Uswisi. Naibu mkurugenzi wa Ofisi ya kupunguza umaskini kwenye Baraza la serikali la China Bw. Chen Zhigang, akihutubia mkutano wa baraza hilo kwa njia video amefahamisha uzoefu na mafanikio ya China katika kupunguza umaskini.

    Bw. Chen amesema chama cha kikomunisti cha China na serikali ya China siku zote wanatoa kipaumbele katika haki za kuishi na kujiendeleza za wananchi, na kuhimiza haki za binadamu kwa njia ya kupunguza umaskini.

    Amejulisha kuwa China inashikilia kanuni ya kujua vyema kwanza watu wanaohitaji msaada, kutekeleza vizuri agizo la kuthibitisha watu wanaobeba majukumu, na mwongozo wa kupunguza umaskini kwa hatua zinazolenga matatizo halisi, na kuweka lengo wazi la kupunguza umaskini. Baada ya juhudi kubwa kuanzia mwaka 2012 hadi 2019, idadi ya watu maskini imepungua kutoka milioni 9.899 hadi kufikia milioni 5.51, miundombinu na uwezo wa utoaji wa huduma za umma zimeboreshwa kwa udhahiri kwenye maeneo yaliyo nyuma kiuchumi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako