• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Marekani yatangaza kuziwekea vikwazo benki 18 za Iran

    (GMT+08:00) 2020-10-09 09:47:44

    Serikali ya Marekani imetangaza kuziwekea vikwazo benki 18 za Iran. Waziri wa mambo ya nje wa Iran Bw. Mohammad Javad Zarif ameilaani Marekani vikali kwa hatua hiyo.

    Waziri wa fedha wa Marekani Bw. Steven Mnuchin jana alitoa taarifa akisema sera ya kuziwekea benki 18 za Iran inaonesha ahadi ya Marekani kuhusu kupiga marufuku kutumia dola za Marekani kwa njia haramu. Kutokana na taarifa hiyo raslimali za benki hizo zilizoko nchini Marekani au zinazodhibitiwa na Marekani zitazuiwa, na raia wa Marekani hawataruhusiwa kufanya biashara na benki hizo. Aidha baada ya muda wa siku 45, shirika lolote la kifedha au mtu yeyote atakayefanya biashara na benki hizo ataweza kuwekwa vikwazo zaidi.

    Waziri wa mambo ya nje wa Iran Bw. Zarif amelaani vikali vikwazo vipya vya Marekani , akisema serikali ya Mareakni inajaribu kukata njia ya malipo ya Iran kwa ajili ya kupata chakula na dawa kutoka nje, wakati wa kipindi cha COVID-19, na njama hiyo ni uhalifu dhidi ya ubinadamu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako