• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mjumbe wa kudumu wa China kwenye UM asisitiza kuhimiza mchakato wa mpito wa Mali

    (GMT+08:00) 2020-10-09 09:54:12

    Mjumbe wa kudumu wa China kwenye Umoja wa Mataifa Bw. Zhang Jun jana katika mkutano wa baraza la usalama kuhusu suala la Mali alitoa hotuba akisisitiza kuhimiza mchakato wa mpito wa Mali.

    Balozi Zhang Jun amesema jumuiya ya kimataifa inafuatilia sana hali ya hivi karibuni iliyotokea nchini Mali, na China inafurahia kuona rais wa mpito wa Mali na makamu wa rais wa Mali wameapishwa na waziri wa mpito pia ameteuliwa. Jumuiya ya uchumi ya nchi za Afrika Magharibi ECOWAS imeamua kuondoa vikwazo dhidi ya Mali. Aidha Mali pia inakabiliana na changamoto nyingi za kurudisha amani na utulivu.

    China inazitaka pande zote za Mali kuendelea kufanya mazungumzo na ushirikiano kwenye msingi wa maslahi ya taifa na raia, kuimarisha maendeleo na kuhimiza mchakato wa mpito kwa utulivu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako