• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • RIADHA: Kibiwott Kandie amtumia salamu Joshua Cheptegei

    (GMT+08:00) 2020-10-09 16:11:47

    Bingwa wa mbio za nyika nchini Kenya, Kibiwott Kandie, amesisitiza kuwa analenga kumzidi maarifa mfalme wa dunia katika mbio za mita 5,000 Joshua Cheptegei ambaye ni raia wa Uganda, kwenye Nusu Marathon ya Dunia itakayofanyika Gydnia, Poland Oktoba 17. Japo nguli wa riadha kutoka Ethiopia, Haile Gebreselassie, anampigia upatu Cheptegei kutamba katika mbio hizo za Poland, Kandie ameshikilia kwamba hana sababu yoyote ya kuhofia. Kandie atalenga kuendeleza matokeo ya kuridhisha yaliyomshuhudia akiibuka mshindi wa RunCzech Half Marathon jijini Prague katika Jamhuri ya Czech Septemba 2020 kwa kutumia dakika 58:38 kwenye kivumbi hicho.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako