• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Takwimu za matumizi katika wiki ya mapumziko ya Siku ya Taifa zaonesha kuwa uchumi wa China unafufuka kwa kasi

  (GMT+08:00) 2020-10-09 17:10:00

  Takwimu za matumizi katika wiki ya mapumziko ya Siku ya Taifa na Sikukuu ya Mbalamwezi iliyoanzia Oktoba 1 hadi Oktoba 8, zinaonesha kuwa uchumi wa China unafufuka kwa kasi, haswa kwenye sekta za utalii, usafiri wa umma, migahawa, manunuzi na burudani.

  Katika wiki hii ya mapumziko ambayo ni likizo ndefu ya kwanza baada ya janga la virusi vya Corona kudhibitiwa nchini China, Bibi Wang na familia yake walikuwa na mpango kamili wa kutalii sehemu mbalimbali na kuwatembelea jamaa na marafiki kwa kutumia usafiri wa treni ya mwendo kasi. Anasema,

  "Napanga kutembelea shule niliyosoma, halafu kujumuika na wanafunzi wenzangu, na pia nitaenda kuhudhuria sherehe ya harusi."

  Takwimu zilizotolewa na Wizara ya Uchukuzi ya China zinaonesha kuwa, kuanzia Oktoba 1 hadi Oktoba 8, abiria milioni 62.11 walisafiri kila siku kwa njia za reli, barabara, anga na majini. Takwimu kutoka Wizara ya Utamaduni na Utalii zinaonesha kuwa, katika mapumziko hayo ya siku nane, sehemu mbalimbali za China kwa ujumla zilipokea watalii wa ndani milioni 637, na kuleta mapato ya Yuan bilioni 466.5, ikiwa ni sawa na dola za kimarekani bilioni 69.5.

  Takwimu zilizotolewa na Wizara ya Biashara ya China zinaonesha kuwa, kuanzia Oktoba 1 hadi Oktoba 8, thamani ya mauzo ya kampuni kubwa za rejareja na chakula na kinywaji yalifikia Yuan trilioni 1.6, na mauzo ya kila siku yaliongezeka kwa asilimia 4.9 ikilinganishwa na mwaka jana kipindi kama hicho.

  Kutazama filamu kwenye majumba ya sinema na kutembelea maonesho mbalimbali ilikuwa ni chaguo la burudani kwa watu wengi katika siku hizo za mapumziko. Kulingana na takwimu za Wizara ya Biashara, katika siku saba za mwanzo thamani ya mauzo ya tiketi katika majumba ya sinema kote nchini ilifikia Yuan bilioni 3.7, ambayo inachukua nafasi ya pili katika historia ya Wiki ya Mapumziko katika miaka ya nyuma.

  Mbali na matumizi yaliyofanywa safarini, matumizi yaliyofanywa kutoka nyumbani pia yaliongezeka kidhahiri. Takwimu zilizotolewa na Idara Kuu ya Posta zinaonesha kuwa, kuanzia Oktoba 1 hadi Oktoba 8, sekta ya posta kwa ujumla ilisafirisha vifurushi bilioni 1.8 ikiwa ni ongezeko la asilimia 62.51 kuliko mwaka jana kipindi kama hiki, na mauzo ya mtandaoni ya bidhaa za chakula, matumizi ya kila siku na vifaa vya kielektroniki yaliongezeka kwa kiasi kikubwa katika kipindi cha mapumziko. Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi wa Soko katika Kituo cha Utafiti wa Maendeleo cha Baraza la Serikali la China Bi. Wang Wei amesema, takwimu hizi zinadhihirisha kuwa uchumi wa China unafufuka kwa kasi.

  "Kuongezeka ghafla kwa matumizi kunaonesha kuwa soko la matumizi nchini China linafufuka kwa kasi, na pia kunaashiria nguvu kubwa ya uhai na uvumbuzi katika soko hilo. Hali hii itatoa msukumo mkubwa kwa ufufukaji imara na maendeleo endelevu ya uchumi wa China katika siku zijazo."

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako