• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China kujiunga na mpango wa utekelezaji wa chanjo ya COVID-19 ni hatua muhimu ya kuihimiza chanjo hicho kuwa bidhaa ya umma

    (GMT+08:00) 2020-10-09 17:39:25

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bi. Hua Chunying leo amesema kuwa, China kujiunga na mpango wa utekelezaji wa chanjo ya COVID-19 ni hatua muhimu ya China kutelekeza ahadi yake ya kuisukuma mbele chanjo hiyo kuwa Bidhaa ya Umma Duniani.

    China jana ilisaini makubaliano na Muungano wa Chanjo Duniani (GAVI) na kujiunga rasmi na mpango wa utekelezaji wa chanjo ya COVID-19. Bi. Hua amesema, hivi sasa virusi vya Corona vimeenea kote duniani, na kutishia usalama wa maisha na afya ya watu wa nchi mbalimbali. China inaahidi kuwa, baada ya utafiti wa chanjo ya China kukamilika na kutumiwa rasmi, chanjo hiyo itatolewa kwa kipaumbele kwa nchi zinazoendelea kama Bidhaa ya Umma Duniani.

    Msemaji huyo amesema China itaendelea kushirikiana na pande mbalimbali za mpango huo, na kutoa mchango wake katika kupambana na virusi vya Corona, na kulinda usalama wa maisha na afya ya watu wa nchi mbalimbali duniani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako