• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Korosho kuwainua wakulima wa Singida

    (GMT+08:00) 2020-10-09 18:23:13

    Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dk. Rehema Nchimbi, amesema zao la korosho lililoanza kulimwa kwa wingi mkoani humo, linatarajia kumaliza umaskini katika eneo hilo na kuwasaidia wakulima kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchini.

    Dk. Nchimbi aliyasema hayo wakati akizungumza na watafiti kutoka Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI), Kituo cha Naliendele wanaoshirikiana na Bodi ya Korosho (CBT), kutoa mafunzo ya kisasa ya kilimo bora cha korosho kwa wakulima ili kuongeza uzalishaji.

    Alisema Mkoa wa Singida kwa miaka ya nyuma ulikuwa ukisemwa ni miongoni mwa mikoa yenye ukame, hivyo waliamua kuanza kushawishi na kwenda pamoja na wakulima kuanza kulima zao la korosho pamoja na mazao mengine na hatimaye mafanikio yameanza kuonekana.

    Alisema wananchi walipewa maeneo hayo kwa kigezo kimoja cha kuhakikisha wanalima korosho na kama wakiacha watapokonywa na mwitikio umekuwa mkubwa hasa katika eneo la Masigati na mashamba hayo yanapanuliwa katika eneo la Itigi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako