• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Vyombo vya habari vya kigeni vyasema kufufuka kwa uchumi wa China kutahimiza maendeleo ya uchumi wa Asia

    (GMT+08:00) 2020-10-09 20:11:32

    Vyombo vya habari vya kigeni vimesema, ukuaji wa uchumi wa China umekuwa na mwelekeo mzuri baada ya kufanikiwa kudhibiti maambukizi ya virusi vya Corona, na kufufuka kwa uchumi wa China kutahimiza maendeleo ya uchumi wa Asia.

    Shirika la Utangazaji la Marekani CNBC limetoa ripoti ikisema, uchumi wa China umefufuka kwa kasi, na sekta ya uzalishaji inastawi, hali ambayo itanufaisha ukuaji wa uchumi wa Asia.

    Shirika la Utangazaji la Uingereza BBC limesema, sekta ya utalii ya China inatarajiwa kufufuka wakati wa sikukuu ya taifa, na hatua ya kuhamasisha matumizi ya ndani na kutoa ruzuku itaharakisha mchakato huo.

    Mwanauchumi mwandamizi wa Shirika la CME la Marekani Blu Putnam amesema, baada ya kudhibiti janga la COVID-19, uchumi wa China umefufuka kwa haraka, na uzoefu mzuri wa China ni kuongeza ujenzi wa miundombinu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako