• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China kutimiza malengo yote ya kutokomeza umaskini vijijini

    (GMT+08:00) 2020-10-12 09:26:23

    Zaidi ya watu milioni 50 vijijini nchini China wameondokana na umaskini katika kipindi cha mpango wa 13 wa maendeleo ya miaka 5, huku kiwango cha umaskini kikipungua kutoka asilimia 4.5 cha mwaka 2016 hadi asilimia 0.6 mwaka 2019, na suala la umaskini wa kikanda limetatuliwa kimsingi.

    Katika kipindi cha mpango wa 13 wa maendeleo ya miaka 5, kipato cha wastani cha watu maskini kimeongezeka kwa asilimia 30 kila mwaka kuanzia mwaka 2016 hadi 2019.

    Vilevile miundo ya kipato cha watu maskini imeboreshwa zaidi, na uwezo wa watu maskini kujiondoa katika umaskini umeongezeka hatua kwa hatua. Watu hao wametimiza lengo la kuondokana na umaskini kwa njia ya kufanya kazi za vibarua na kujishughulisha na uzalishaji mali.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako