• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Marais wa China na Senegal watoa salamu za pamoja kuadhimisha miaka 20 tangu kuanzishwa kwa FOCAC

    (GMT+08:00) 2020-10-12 10:40:08

    Rais Xi Jinping wa China na rais Macky Sall wa Senegal ambayo ni nchi mwenyekiti wa upande wa Afrika wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) wametoa salamu za pamoja kuadhimisha miaka 20 tangu kuanzishwa kwa Baraza hilo.

    Kwenye salamu hizo, marais hao wamesema katika miaka 20 iliyopita, kutokana na juhudi za pamoja za China na nchi za Afrika, FOCAC imekuwa jukwaa muhimu la kufanya mazungumzo, na mfumo wenye ufanisi wa kufanya ushirikiano kati ya pande hizo mbili, na pia limekuwa bendera muhimu ya ushirikiano kati ya nchi za kusini.

    Marais hao pia wamesema, janga la COVID-19 ni changamoto kubwa inayokabili binadamu, na kuleta athari kubwa kwa uchumi wa dunia. China na Afrika zinapenda kushikamana na kushirikiana ili kukabiliana kwa pamoja na aina zote za matishio na changamoto, na kuufanya ushirikiano kati yao uwe mfano mzuri wa utaratibu wa pande nyingi na mafanikio ya pamoja.

    Aidha, wamesisitiza kuwa China na Afrika zitahimiza uhusiano wao wa wenzi wa kimkakati wa pande zote ufikie kiwango cha juu zaidi, kujenga jumuiya ya binadamu yenye hatma ya pamoja, ili kuwanufaisha watu wa pande hizo mbili na kuanzisha mustakabali mzuri wa binadamu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako