• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Taifa Stars ya Tanzania yashindwa kutamba mbele ya Warundi

    (GMT+08:00) 2020-10-12 16:59:54

    TIMU ya Taifa Tanzania ya Tanzania jana ilipoteza kwa kufungwa bao 1-0 kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Burundi uliochezwa Uwanja wa Mkapa. Kwenye mchezo wa huo ambao mgeni rasmi alikuwa ni Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kipindi cha kwanza timu zote mbili zilitoshana nguvu baada ya kwenda vyumba vya kubadilishia nguo wakiwa hawajafungana. Kipindi cha pili mambo yalizidi kuwa magumu kwa timu zote mbili ambapo Stars ilijaribu kufanya mashambulizi yaliyoshindwa kuzaa matunda na Burundi ilikuwa ya kwanza kupiga shuti la kwanza ambalo lililenga lango kipindi cha pili. Bao pekee la ushindi lilipatikana dakika ya 84 kupitia kwa Said Ntibazonkiza na kuwafanya Burundi kuibuka na ushindi ugenini. Simon Msuva nyota wa timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars amesema kuwa haikuwa bahati kwao kwa kuwa walipambana ili kupata ushindi ila mambo yalikuwa magumu kwao. Stars ilimaliza dakika 90 ikiwa pungufu baada ya kiungo mkabaji Jonas Mkude kuonyeshwa kadi nyekundu dakika ya 78 kwa kuwa alikuwa ameonyeshwa kadi mbili za njano.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako