• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Kibarua cha kocha Solskjaer chaanza kuchomoza mbawa kwa mbali

    (GMT+08:00) 2020-10-12 17:03:41

    Kwa mujibu wa taarifa kutoka The Mirror Makamu Mwenyekiti Mtendaji Ed Woodwars yupo tayari kumtimua kazi kocha Ole Gunnar Solskjaer kama klabu hiyo itaendelea kupata matokeo mabovu. Manchester United imepoteza mechi mbili za kwanza za Ligi Kuu England. Taarifa zinadai kuwa kocha wa zamani wa Spurs, Mauricio Pochettino anatajwa kuwa mrithi wake ndani ya Old Trafford. Solskjaer amekuwa kocha wa Man United tangu Machi 2018 baada ya kuwa na mwenendo mzuri alipokuwa kocha wa muda. Aliiongoza Man United kumaliza katika nafasi ya nne na kufika nusu fainali ya Ligi ya Europa msimu uliopita. Lakini kocha huyo mwenye miaka 47 amekuwa na wakati mgumu kwasasa kutokana na kuanza vibaya msimu mpya. Kipigo cha mabao 3-1 dhidi ya Crystal Palace katika mchezo wake wa kwanza wa ligi kilifuatiwa na ushindi wa 3-2 dhidi ya Brighton. Na aliwajibika katika kipigo cha mabao 6-1 dhidi ya Tottenham mapema mwezi huu. Solskjaer, ambaye ana mkataba na Man United hadi 2022, anakabilana na mwezi mgumu kwake. Man United itavaana na Newcastle na Chelsea katika michezo ya Ligi Kuu England, kabla ya kucheza na Paris SaintGermain katika Ligi ya Mabingwa Ulaya baadaye mwaka huu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako