• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Shenzhen yajengwa kuwa mji wa kivumbuzi nchini China

    (GMT+08:00) 2020-10-12 17:17:12

    Mji wa Shenzhen likiwa eneo maalumu la kwanza la kiuchumi nchini China, tangu lilipoanzishwa miaka 40 iliyopita, umekuwa ukipiga hatua mbele kwenye mchakato wa kufanya mageuzi na ufunguaji mlango, na maendeleo ya kiuchumi.

    Mwezi Agosti mwaka 2019, serikali ya China ilifanya uamuzi muhimu wa kuunga mkono kuujenga mji wa Shenzhen kuwa eneo la kielelezo cha ujamaa wenye umaalumu wa China. Ukidhihirisha kuwa, ifikapo mwaka 2025, Shenzhen itajengwa kuwa mji wa kivumbuzi wa kisasa wa kimataifa, na ifikapo mwaka 2035, itajengwa kuwa mji wenye ushawishi mkubwa duniani, na ifikapo katikati ya karne hii, itajengwa kuwa mji wa mfano mzuri wa kuigwa duniani ambao una uwezo mkubwa wa ushindani, uvumbuzi na ushawishi mkubwa duniani.

    Hivi sasa Shenzhen ina njia 219 za safari za meli za kimataifa zinazobeba makontena, ambazo zinaelekea bandari zaidi ya 300 kwenye nchi na sehemu zaidi ya 100, thamani ya jumla ya biashara ya nje imekuwa ikishika nafasi ya kwanza kati ya miji mikubwa na ya kati nchini China kwa miaka 27 mfululizo. Katika mtaa wa Shekou mjini Shenzhen, bandari moja inayotumia teknolojia ya 5G ambayo ina uwezo wa kuchukua tani laki 2 imeanza kutumiwa.

    Tokea mwaka huu, Shenzhen imetekeleza hatua 210 za mageuzi za kuboresha mazingira ya biashara katika sekta 14, ili kuweka mazingira mazuri zaidi ya biashara ya kimataifa. Hivi sasa makampuni karibu 300 ambayo yanashika nafasi 500 za mwanzo duniani yamewekeza mjini humo, Shirikisho kuu la viwanda na wafanyabiashara la Ujerumani, na Shirikisho la Biashara kati ya Uingereza na China pia yameanzisha ofisi mjini Shenzhen. Kuanzia mwezi Januari hadi Julai mwaka huu, matumizi ya fedha za kigeni ya Shenzhen yamekaribia dola za kimarekani bilioni 4.9, likiwa ongezeko la asilimia 12.8. Mkurugenzi wa Chama cha wafanyabiashara wa Marekani nchini China Bw. Alan Beebe ameeleza kuwa Shenzhen ina miundo mbinu mizuri na ya aina mbalimbali, ambapo mashirika mengi mazuri ya sayansi na teknolojia yamejenga kwa pamoja mfumo mzuri wa ikolojia, na kuufanya mji huo uwe na mvuto mkubwa.

    Mkurugenzi mkuu wa Baraza la uchumi la dunia Bw. Borge Brende anaona kuwa, chini ya uongozi wa rais Xi Jinping wa China, Shenzhen itapata maendeleo mapya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako