• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • TANZANIA : WAZALISHAJI SARUJI WALIA KERO YA TOZO

    (GMT+08:00) 2020-10-12 17:34:47

    Kampuni za uzalishaji saruji na mbolea nchini, zimeomba tozo ya usafirishaji ambayo inatozwa na wizara tatu, itozwe na wizara moja ili kupunguza bei ya bidhaa hizo kwa wananchi. Kampuni hizo ni Dangote, Twiga, Tanga, Mbeya, Lake, Maweni Limestone na Minjingu. Kampuni hizi tayari zimekutana na Katibu mkuu wa Wizara ya Madini, Prof. Simon Msanjila, na kujadili tozo mbalimbali za usafirishaji na ukaguzi.

    Wakizungumza walipokutana na Katibu huyo mkuu, wawakilishi wa kampuni hizo walisema tozo ya usafirishaji inatozwa na wizara za madini, kilimo na viwanda na biashara, na imekuwa kero kwao na kuiomba wizara ya Madini, tozo hiyo ielekezwe kwenye wizara moja na tozo ya ukaguzi ifutwe au ipunguzwe.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako