• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mwenyekiti wa kamati ya Umoja wa Ulaya akaribisha China kujiunga kwenye mpango wa COVAX

    (GMT+08:00) 2020-10-12 19:06:09

    Mwenyekiti wa kamati ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leye jana kwenye tovuti ya mtandao wa kijamii amesema, anakaribisha China kujiunga kwenye mpango wa utekelezaji wa chanjo ya COVID-19. Amesema, Umoja wa Ulaya na China zina lengo moja, utaratibu wa pande nyingi ni muhimu kwa chanjo kunufaisha sehemu zote, na kuwafanya watu wote wenye mahitaji wapate chanjo. Anatarajia China na wenzi wake watashirikiana kuanzia sasa.

    Siku hiyo hiyo, mjumbe mwandamizi wa Umoja wa Ulaya anayeshughulikia mambo ya nje na sera za usalama Josef Borell pia amepongeza uamuzi huo wa China katika tovuti ya mtandao wa kijamii, akisema ni juhudi na ahadi za dunia nzima ndio njia pekee ya kupata ushindi wa mapambano dhidi ya maambukizi ya virusi vya Corona.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako