• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wachumi wawili kugawa Tuzo ya Uchumi ya Nobel mwaka 2020

    (GMT+08:00) 2020-10-12 19:40:38
    Chuo cha Sayansi cha Royal Swedish leo Jumatatu kimetoa taarifa kikitangaza kuwa Wachumi Paul R. Milgrom na Robert B. Wilson wametunikiwa Tuzo ya Uchumi ya Nobel mwaka 2020 kwa "kuboresha nadharia ya mnada na uvumbuzi wa muundo mpya wa mnada".
    Taarifa hiyo imebainisha kuwa Milgrom na Wilson wamesoma mnada unavyofanya kazi, na kutumia maarifa yao kuweka muundo mpya wa mnada wa bidhaa na huduma ambazo ni vigumu kuuza kwa njia iliyozoeleka zamani, kama vile mawimbi ya redio. Ugunduzi wao umewanufaisha wauzaji, wanunuzi na walipa kodi duniani.
    Zawadi ya tuzo hiyo ambayo ni dola za kimarekani milioni 1.14 itagawiwa sawa kwa wachumi hao wawili.
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako