• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mama Peng Liyuan apongeza tuzo ya elimu kwa watoto wa kike na wanawake ya UNESCO

    (GMT+08:00) 2020-10-12 21:17:14
    Mke wa rais Xi Jinping wa China, na mjumbe maalumu wa kuhimiza elimu ya watoto wa kike na wanawake kwenye Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa UNESCO, Mama Peng Liyuan, ametoa salamu za pongezi kwa njia ya video kwenye tuzo ya elimu kwa watoto wa kike na wanawake ya UNESCO. Mama peng ametoa salamu za pongezi kwa watu waliopewa tuzo hiyo kutoka Sri Lanka na Kenya, na kusema kuwa amesema China itaendelea kuhimiza mawasiliano na ushirikiano wa elimu ya kimataifa, na kutoa mchango mkubwa zaidi kwa ajili ya kuhimiza elimu ya watoto wa kike na wanawake, na kutimiza malengo ya maendeleo endelevu ya Umoja wa Mataifa ya mwaka 2030. Katibu mkuu wa UNESCO Bibi Audrey Azoulay amesifu na kuishukuru serikali ya China kwa kuunga mkono tuzo hiyo, na kusisitiza kuwa shirika hilo linapenda kushirikiana na pande mbalimbali, kuhimiza watoto wa kike na wanawake duniani kupata fursa sawa za elimu na mustakabali mzuri.
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako