• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mji wa Qingdao wawapima wakazi wote virusi vya Corona baada ya maambukizi mapya kuibuka

    (GMT+08:00) 2020-10-13 08:42:47

    Mji wa Qingdao mkoani Shandong, mashariki mwa China umeanza kupima virusi vya Corona kwa wakazi wote baada ya maambukizi mapya kuripotiwa.

    Ofisa habari wa serikali ya Qingdao amesema, mpaka sasa mji huo umemaliza kazi ya kupima au kuchukua sampuli kwa watu zaidi ya milioni moja, na hakuna maambukizi mapya yaliyogunduliwa miongoni mwa watu laki 3.1 ambao majibu yao ya upimaji yametolewa, na kuongeza kuwa, upimaji kwa wakazi wote wa mji huo unatarajiwa kumalizika ndani ya siku tano.

    Uchunguzi umeonesha kuwa watu watatu wasio na dalili walihusiana na hospitali ya magonjwa ya kifua ya Qingdao, ambayo iliweka maeneo maalumu ya kutibu watu walioambukizwa kutoka nje ya nchi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako