• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • AU yaondoa vikwazo dhidi ya Mali kutokana na hali ya usalama kuboreka

    (GMT+08:00) 2020-10-13 08:58:25

    Kamati ya Umoja wa Afrika (AU) imetangaza jana kuwa imeondoa vikwazo dhidi ya Mali vya kutoshiriki kwenye shughuli zozote za Umoja baada ya hali nchini humo kuboreka.

    Uamuzi huo ulifikiwa na Kamati ya Amani na Usalama ya Tume ya Umoja wa Afrika katika mkutano wake uliofanyika hivi karibuni uliozungumzia hali ya sasa nchini Mali.

    Kamati hiyo pia imepongeza kuachiliwa kwa wafungwa wa kisiasa waliokamatwa Agosti 18, akiwemo rais wa zamani wa nchi hiyo Ibrahim Boubacar Keita, na kuitaka Serikali ya Mpito kuongeza juhudi na nia ya kutekeleza utaratibu wote wa mpito, ikiwemo kuanzisha kwa wakati Baraza la Kitaifa la Mpito.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako