• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mjumbe wa China asema sio haki kuitaka nchi hiyo ishiriki katika majadiliano ya pande tatu ya udhibiti wa silaha

    (GMT+08:00) 2020-10-13 08:58:47

    Mkuu wa ujumbe wa China na kaimu mwakilishi wa China katika Umoja wa Mataifa, Balozi Geng Shuang amesema, sio haki kuitaka China kushiriki kwenye majadiliano ya pande tatu ya udhibiti wa silaha.

    Katika taarifa yake iliyotolewa kwenye mjadala wa kawaida wa Kamati ya Kwanza ya mkutano wa 75 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, Balozi Geng amepinga kile kilichoitwa 'mjadala wa pande tatu wa udhiniti wa silaha' uliopendekezwa na Marekani hivi karibuni. Amesema Marekani imeitaja China kama nchi ya tatu ya nguvu za nyuklia duniani, kuzusha uvumi kuhusu mashindano ya silaha za nyuklia kati ya Marekani, Russia na China, na kupendekeza 'mjadala wa pande tatu wa udhibiti wa silaha.'

    Balozi Geng amesema, hatua hiyo ya Marekani ni kuondoa ufuatiliaji wa jamii ya kimataifa, na inalenga kutafuta sababu ya Marekani kukwepa wajibu wake wa kimsingi wa kuondoa silaha za nyuklia.

    Balozi Geng ameongeza kuwa, China inaendeleza mkakati wa nyuklia kwa ajili ya kujilinda, na daima inashikilia uwezo wake wa kinyuklia katika ngazi ya chini inayohitajika kwa ajili ya usalama wa taifa, na kamwe haitashiriki kwenye mashindano ya silaha za nyuklia na nchi nyingine yoyote.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako