• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yaahidi kuisaidia Sudan Kusini kukabiliana na maafa

    (GMT+08:00) 2020-10-13 09:04:33

    Serikali ya China imeahidi kutoa msaada wa dola 300,000 za Kimarekani kwa Sudan Kusini kukabiliana na maafa inayoikabili nchi hiyo.

    Balozi wa China nchini Sudan Kusini Hua Ning ametoa ahadi hiyo alipokutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Sudan Kusini Beatrice Khamisa Wani.

    Balozi Hua amesema, msaada huo utaisaidia Sudan Kusini kukabiliana na mafuriko yaliyowaathiri watu laki 8 nchini humo, na kwamba China itaendelea kushirikiana na Sudan Kusini kuimarisha mawasiliano na ushirikiano katika nyanja mbalimbali wakati nchi hizo mbili zikisherehekea miaka 10 tangu zianzishe uhusiano wa kibalozi.

    Kwa upande wake, Bi. Khamisa ameishukuru serikali ya China na watu wake kwa kutoa msaada wakati Sudan Kusini inapokumbwa na mafuriko, na kuongeza kuwa nchi hiyo itaimarisha uhusiano na China ili kuwanufaisha watu wa nchi hizo mbili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako