• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Rick Parry apongeza mageuzi Ligi Kuu ya Uingereza

    (GMT+08:00) 2020-10-13 16:50:02

    Mwenyekiti wa Ligi ya Uingereza, Rick Parry amezisifu klabu za Liverpool na Manchester United kwa 'kuonyesha uongozi' baada ya kuibuka na mpango wa kufanya mageuzi makubwa ya Ligi Kuu, ambayo anaamini yataunufaisha mchezo huo. Mpango huo tata wa 'Project Big Picture' (Mradi wa Mtazamo Mpana) unajumuisha mapendekezo ya kupunguza timu za Ligi Kuu kutoka 20 hadi 18 na kufuta michuano ya Kombe la Ligi na mechi ya Ngao ya Jamii. Klabu itakayomaliza msimu ikishika nafasi ya 16 katika Ligi Kuu itaingia katika michuano ya mtoano pamoja na timu za daraja la kwanza, wakati kutakuwa na haki pana zaidi za kupiga kura kwa klabu tisa zilizocheza Ligi Kuu kwa muda mrefu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako