• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Kante ataka kuondoka Chelsea

    (GMT+08:00) 2020-10-13 16:50:23

    Kiungo wa Klabu ya Chelsea raia wa Ufaransa, N'Golo Kante anaweza kuondoka ndani ya timu hiyo mwezi Januari baada ya kuzozana na Kocha Mkuu, Frank Lampard baada ya kugomea kumpa ruhusa ya kwenda kwenye sherehe ya ndoa ya rafikiyei. Kiungo huyo ambaye ni miongoni mwa wanaofanya vizuri duniani kwa sasa na ndani ya timu yake ya Taifa ya Ufaransa kwa sasa yupo kwenye majukumu yake ya timu ya taifa.

    Ripoti zinaeleza kuwa Lampard aligomea ishu ya Kante kuacha mafunzo kwa muda na kuhudhuria sherehe ya harusi ya rafikiye kabla ya mapumziko mafupi yaliyotokana na timu za taifa kuwa kwenye majukumu. Ripoti zinaeleza kuwa kiungo huyo mwenye miaka 29 anaweza kuibukia ndani ya Klabu ya Real Madrid ambayo inashiriki La Liga kwa kuwa ni timu ambayo anaipenda iwapo ataondoka ndani ya Stamford Bridge Kante hakuanza mazoezi pamoja na wachezaji wenzake mwanzoni mwa msimu kwa kuwa alianza kukaa karantini kutokana na hofu ya kwamba ana maambukizi ya Virusi vya Corona.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako