• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • GSM awa Mwenyekiti wa Kamati ya Ushindi Taifa Stars

    (GMT+08:00) 2020-10-13 16:51:24

    Rais wa TFF Wallace Karia amemteua Ghalib Said Mohamed (GSM) kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Ushindi ya Taifa Stars, Makamu Mwenyekiti ni Salim Abdallah, na katibu wa kamati hiyo ni Eng Hersi Said. Kamati hiyo inalenga kusaidia hamasa na ushindi kwa Taifa ili kuiwezesha kufuzu tena michuano ya AFCON kwa kushinda mechi zake za kuwania kufuzu ikiwemo dhidi ya Tunisia. Wakati huohuo nyota wa Burundi Said Ntibazonkiza aliyeifunga Taifa Stars juzi katika mchezo wa kirafiki Burundi dhidi ya Tanzania "'Taifa Stars" amesajiliwa na Yanga SC. Inaripotiwa ni mkataba wa miezi 18 na ataungana na timu hiyo mwishoni mwa mwezi Novemba. Yanga SC sasa kwa kushirikiana na mdhamini na kit suplier wao kampuni ya GSM wamedhamiria kuboresha timu hiyo baada ya kuendelea kusajili wachezaji wa kigeni na majina makubwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako