• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Zimbabwe yasajili ongezeko kubwa la wageni kwenye uwanja mkuu wa ndege

    (GMT+08:00) 2020-10-13 17:10:53

    Zimbabwe imesajili ongezeko kubwa la idadi ya wageni kwenye uwanja wake mkuu wa ndege tangu kuanzishwa tena kwa safari za ndege za kimataifa mwanzoni mwa mwezi huu.

    Tawanda Gusha, ambaye ni Mkurugenzi wa Huduma za Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Robert Gabriel Mugabe, amesema ndege zinazotua kwenye uwanja wa ndege zimebeba asilimia 30 ya abiria, huku ndege za kikanda zikijaza ndege nzima.

    Ndege zilizoanza kutua Oktoba Mosi kwenye uwanja huo wa ndege ni pamoja na za Shirika la Ndege Kenya, Afrika Kusini na Fastjet. Wakati huohuo waziri wa Habari, Uenezi na Huduma za utangazaji Monica Mutsvangwa amesema serikali ya Zimbabwe inaweka umuhimu mkubwa kwenye usalama wa abiria na wafanyakazi wa mashirika ya ndege kutokana na janga la COVID-19.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako