• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Thamani ya jumla ya uagizaji na uuzaji bidhaa nje ya China yaongezeka kwa mara ya kwanza mwaka huu

    (GMT+08:00) 2020-10-13 18:04:23

    Takwimu kutoka Idara kuu ya forodha ya China zimeonesha kuwa, katika robo tatu za mwanzo mwaka huu, thamani ya uagizaji na uuzaji bidhaa nje ya China imekuwa kubwa zaidi kuliko ilivyotarajiwa, na kufikia RMB yuan trilioni 23.12, sawa na dola za kimarekani trilioni 3.4, likiwa ni ongezeko la asilimia 0.7 kuliko mwaka jana wakati kama huu, na thamani ya jumla ya uagizaji na uuzaji bidhaa nje ya China imeongezeka kwa mara ya kwanza mwaka huu.

    Kwa mujibu wa takwimu kutoka Idara kuu ya Forodha, tokea mwaka huu thamani ya uagizaji na uuzaji bidhaa nje ya China imerejea katika hali yenye utulivu. Msemaji wa idara hiyo, na mkurugenzi wa Idara ya uchambuzi wa takwimu Bw. Li Kuiwen anasema:

    "Thamani ya biashara imeongezeka kwa zaidi ya yuan trilioni 1 katika robo ya pili na ya tatu mwaka huu, sawa na dola za kimarekani milioni 15, likiwa ni ongezeko zaidi ya asilimia 10. Katika robo ya tatu, thamani ya jumla ya uagizaji na uuzaji bidhaa nje, thamani ya jumla ya uuzaji bidhaa nje, na ile ya uagizaji wa bidhaa kutoka nje zote zimeweka rekodi mpya katika historia."

    Takwimu zimeonesha kuwa thamani ya uuzaji bidhaa nje ya China imedumisha ongezeko kwa miezi sita mfululizo. Bw. Li akifahamisha sababu tatu muhimu ya hali hiyo anasema:

    "Kwanza vifaa vya kujikinga na virusi vya Corona vimechangia ongezeko la asilimia 2.2. Pili bidhaa zinazotumiwa nyumbani zikiwemo Laptop, kompyuta ,na vifaa vya nyumbani, zimechangia ongezeko la asilimia 1.1. Tatu, kurejeshwa kwa uzalishaji nchini kumeleta ongezeko la oda ya uuzaji wa bidhaa nje."

    Bw. Li pia ameeleza kuwa, uuzaji wa bidhaa wa China kwa wenzi muhimu wakiwemo Umoja wa Nchi za Asia Mashariki, Umoja wa Ulaya, Marekani, Japan na Korea Kusini umedumisha ongezeko, na Umoja wa Nchi za Asia Mashariki umekuwa mwenzi mkubwa wa kwanza wa biashara kwa China.

    Mbali na hayo Bw. Li amesisitiza kuwa, hivi sasa maendeleo ya biashara nje ya China yanakabiliwa na hali yenye utatanishi mkubwa, lakini mwelekeo wa kupata maendeleo katika muda mrefu ujao haubadiliki.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako