• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Nigeria atafuta uungaji mkono wa kimataifa kwa mgombea wa WTO kutoka Nigeria

    (GMT+08:00) 2020-10-13 18:15:13

    Rais Muhammadu Buhari wa Nigeria jana alisisitiza kuwa anatafuta uungaji mkono wa kimataifa ili kuhakikisha Bibi Ngozi Okonjo-Iweala ambaye ni waziri wa zamani wa fedha wa nchi hiyo anashinda kwenye kinyang'anyiro cha mkurugenzi mkuu mpya wa Shirika la Biashara Duniani WTO.

    Rais Buhari alikutana na Bibi Okonjo-Iweala katika Ikulu ya Nigeria akiahidi kuwa Nigeria itatafuta kila fursa na kufanya juhudi zote ili ashinde kwenye uchaguzi wa WTO.

    Rais Buhari alisema kuwa atawapigia simu na kutuma barua zaidi kwa viongozi wa nchi mbalimbali ili kuomba msaada zaidi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako