• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Idadi ya watu wanaokufa kwa Corona nchini Marekani huenda ikafikia laki 4 hadi kufikia Februari mwakani

    (GMT+08:00) 2020-10-13 18:15:54

    Taasisi ya tathmini ya takwimu ya afya ya Chuo Kikuu cha Washington nchini Marekani ilitoa makadirio mapya ya janga la COVID-19 ikisema kuwa, kutokana na mwelekeo wa mwenendo ya janga hilo, hadi kufikia mwezi Februari mwaka kesho idadi ya watu wanaokufa kutokana na virusi vya Corona huenda itafikia laki 4.

    Makadirio hayo yanaonesha kuwa, kama Marekani ikipunguza hatua za udhibiti na kinga, idadi ya watu wanaokufa itazidi laki 5, na kama asilimia 95 ya watu wakiweza kuendelea kuvaa barakoa, idadi ya watu wanaokufa kutokana na virusi vya Corona itafikia laki 3.15.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako